
Asante
Written by Paddy Daniel & Paddy Amissi
Asante is Swahili for “thank you.” A song of gratitude for a God who loved us before we knew Him — rain in the middle of the desert, every single day.
Verse 1
Ulinipenda kabla sijakujua
Ulinithamini bila ya ombi wala dua
Mnyunyizi wangu kati ukame na jua
Uzima kati ya jangwa wanipa mvua
Kila siku inanyesha inanyesha, inanyesha
Ya Baraka waninywesha waninywesha, waninywesha
Sina hofu na kesho
Ya noma jana ulini-show
Ya kati yote ni pasho
Maana wewe ni Mwanzo na Mwisho
Chorus
Nasema asante
(Kwa upendo wako na rehema zako Abba)
Nasema asante
(Kwa fadhili zako zidumuzo milele na milele)
Nasema asante, asante (Umenipenda bure bure)
Nasema asante, asante (Kwa kunipea nafasi)
Verse 2
Ona ona ona
Vile umenitendea
Kila kona nakuona, ona
Pendo lako laenea
You bless me daily, I can’t hide it
Bwana wewe wanipendelea
Milimani, mabondeni
Wewe ukiwa nami
Siku zote nasherekea
Pre-chorus
Sina hofu na kesho
Ya noma jana ulini-show
Ya kati yote ni pasho
Maana we ni Mwanzo na Mwisho
Chorus
Nasema asante
(Kwa upendo wako na rehema zako Abba)
Nasema asante
(Kwa fadhili zako zidumuzo milele na milele)
Nasema asante, asante (De m’avoir protégé)
Nasema asante, asante (Je te remercierai éternellement, Papa)